Papa ameombea nchi pendwa ya myanmar ili vurugu ziishe - | vatican news

Papa ameombea nchi pendwa ya myanmar ili vurugu ziishe - | vatican news

Play all audios:

Loading...

Papa Francisko amemwomba Mungu ili uchungu na vifo nchi Myanmar viishe na watu wasitoe machozi kamwe na mategemeo kuwa wakazi wake wanaweza kufanya kazi pamoja kwa amani.Maombi hayo ni mara


baada ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika 3 Oktoba 2021,pamoja na waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro. NA SR. ANGELA RWEZAULA - VATICAN.  Papa Francisko Dominika


tarehe 3 Oktoba 2021, mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana ameonesha hisia za huruma na kuombea nchi ya bara la Asia ya Mynamar ambayo, habari za ghasia na vurugu zinaendelea


kusikika. "Ninaomba Mungu kwa upya zawadi ya amani kwa ajili ya ardhi pendwa ya Myanmar", amesema Papa. Matashi ya Baba Mtakatifu ni kwamba mikono ya wakazi wa nchi hiyo isifute


machozi tena ya uchungu na vifo, walakini waweze kukumbatiana na kushikana mikono kwa ajili ya kushinda matatizo na kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya wakati ujao wa amani. NCHINI MYANMAR


SASA NI MIEZI NANE TANGU KUTOKEA KWA MAPANDUZI YA KIJESHI YA SERIKALI MNAMO TAREHE MOSI FEBRUARI, AMBAPO HABARI ZINAZOFIKA NI mbaya sana za ukandamizaji wa utawala wa kijeshi ulioko


madarakani ambao unafyatua risasi za moto dhidi ya waandamanaji ambao wanangia barabarani katika miezi ya hivi karibuni kupinga hatua  ya ukosefu wa demokrasia na hutumiaji wa silaha nzito


na helikopta dhidi ya vijiji. Wakuu wa serikali kivuli ya umoja wa kitaifa (NUG), mwezi uliopita walitangaza vita ya kupiga maarufu vya kujihami dhidi  ya mapinduzi, wakitoa wito kwa vikundi


vyote vyenye silaha nchini na demokrasia yote ya Birimania ambapo shukrani kwa kuzinduliwa kwa kampeni ya mafunzo ya kijeshi, kujiunga na Vikosi vyao vya Ulinzi vya Wananchi (Pdf)


iliyoundwa mwezi Mei. Wakimbizi wa Rohingya nchini Myanmar BABA MTAKATIFU FRANCISKO, AIDHA AMESEMA: “LEO, HUKO CATANZARO, MARIA ANTONIA Samà na Gaetana Tolomeo, wanawake wawili waliolazimika


kutoamka kimwili katika maisha yao yote, wametangazwa kuwa wenyeheri. Wakisaidiwa na neema ya kimungu, waliukumbatia msalaba wa udhaifu wao, wakibadilisha maumivu kuwa sifa kwa Bwana.


Kitanda chao kikawa kielelezo cha kiroho na mahali pa sala na ukuaji wa Kikristo kwa watu wengi ambao walipata faraja na matumaini huko. Tuwapigie a makofi wenyeheri wapya… Mwenyeheri


Gaetana Tolomeo Mwenyeheri Antonia Sama AKIENDELEA PAPA FRANCISKO AMESEMA KUWA "JUMAPILI HII YA KWANZA YA OKTOBA, MAWAZO YANAWAENDEA WAAMINI WALIOKUSANYIKA KWENYE MADHABAHU ya Pompei


ili kusali Maombi kwa Bikira Maria. Katika mwezi huu tujibidishe na tusasishe pamoja kujitoa kusali Rozari Takatifu". Wakati wa Maombi kwa Bikira Maria wa Pompei