Papa baada ya kufika ameshukuru kwa bikira maria mkuu - | vatican news

Papa baada ya kufika ameshukuru kwa bikira maria mkuu - | vatican news

Play all audios:

Loading...

Papa baada ya kurudi kutoka Hungaria,kama kawaida ya kila Ziara yake ya Kitume,alikwenda moja kwa moja kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kwa kukaa kitambo kwa sala mbele ya Picha ya


Bikira Salus Populi Romani.Baadaye alirudi mjini Vatican. NA ANGELLA RWEZAULA; - VATICAN. Baba Mtakatifu Francisko, Dominika jioni tarehe 30 Aprili 2023, alitua katika Uwanja wa Ndege


Kimataifa wa Fiumicino, Roma, majira ya saa 1.25 usiku, akiwa anarejea kutoka ziara yake ya 41 ya kitume jijini Budapest nchini Hungaria, iliyoanza Ijumaa tarehe 28 Aprili 2023. Kwa hiyo


kama alivyofanya kabla ya kuondoka, ambavyo pia ni kawaida yake mwishoni mwa kila ziara, Baba Mtakatifu Francisko alikwenda kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, Roma  ili  kumshukuru


Bikira kwa ajili mafanikio ya siku tatu za ziara hiyo ambazo zimemwona akifanya mikutano mbalimbali huko Budapest. Ni taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican. Katika


taarifa hiyo inabainisha kwamba, Baba Mtakatifu alitulia katika maombi kwa dakika chache mbele ya picha ya  Bikira ‘Salus Populi Romani’, yaani Afya ya Watu wa Roma. Hifuatayo ni video fupi


inayoelezea ziara hii ya Papa Francisko katika siku ya mwisho wa siku tatu za kina katika nchi ya Hungaria aliyoanza tarehe 28 hadi 30 Aprili 2023. [embedded content] Ziara ya kitume nchini


Hungaria: siku yake ya mwisho Ikumbukwe, katika ziara yake ya 41 ya kitume, Baba Mtakatifu alipowasili katika uwanja ndege wa kimataifa wa Budapest 28 Aprili, alipokelewa na Balozi wa


Vatican; baadaye kulikuwa na wakati wa kukaribishwa rasmi katika uwanja wa Jumba la ‘Sándor’,(yaani Ikulu) ambayo ni makazi ya rais wa Hungaria, Bi Katalin Éva Novák. Kulifuatia mikutano ya


itifaki kuanzia na  mkuu wa nchi, Waziri Mkuu Viktor Orban na mamlaka na wawakilishi wa mashirika ya kiraia na mashirika ya kidiplomasia. Siku hiyo ilifungwa saa kumi na moja jioni ambapo


Papa alikutana na wakleri, watawa na waseminari katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano. Ziara ya Papa nchini Hungaria   (Vatican Media) Jumamosi tarehe 29 Aprili alifanya ziara ya kibinafsi


 ya faragha  kwa watoto vipofu ambao ni wageni wa taasisi ya Mwenyeheri László Batthyány-Strattmann  iliyopewa jina la daktari wa macho wa Hungaria wakati wa kutangazwa mwenyeheri mnamo


mwaka 2003,  ikifuatiwa na mkutano na maskini na wakimbizi katika Kanisa la Mtakatifu Elizabeth wa Hungaria. Baada ya hapo alitembelea Jumuiya ya Kikatoliki -kigiriki. Mikutano mingine


alasili,  ilikuwa ni mkutano na vijana katika Uwanja mkubwa wa mchezo liitwalo  László Papp Budapest na saa 12.00 jioni katika Ubalozi wa Vatican nchini humo, alifanya mkutano wa faragha na


wanashrika wa  Shirika Kijesuit. Lakini pia Papa alikutana na kiongozi wa Kiorthodox, Hilarion. Ziara ya Papa   (VATICAN MEDIA Divisione Foto) Dominika tarehe 30 Aprili 2023  ameadhimisha  


Misa Takatifu, katika Uwanja wa Kossuth Lajos jijini Budapest na baada ya misa alitoa wito na Sala ya Malkia wa Mbingu,  na  hatimaye mkutano alasiri ulikuwa ni mktano wa ulimwengu wa chuo


kikuu na utamaduni kabla ya kuondoka kurudi Vatican.  Hotuba ya Papa   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)