Play all audios:
Mvutano wa kibiashara uliongezeka wiki hii baada ya Brussels kutangaza ushuru wa thamani ya euro bilioni 26 kwa bidhaa za Marekani, kujibu ushuru wa asilimia 25 uliowekwa na utawala wa Trump
kwa chuma na alumini. Vita vya ushuru kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani vinaendelea kupanuka, huku wachambuzi wakionya kuwa hali hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa uchumi wa
pande zote mbili. Cecilia Malmström, aliyewahi kuwa Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya, anasema kuwa hakuna mshindi katika vita vya kibiashara. Malmström alisema ni mchezo wa kupoteza
kwa pande zote, na kuongeza kuwa wale walioko katika hatari ya kupoteza zaidi ni wateja na watu wa kawaida kwa sababu bei zinapanda, na hivyo kuathiri mfumuko wa bei, ajira na ukuaji. Soma
pia:Canada yaahidi kushinda vita vya kibiashara dhidi ya US Huku ushuru mpya ukitarajiwa kutoka kwa utawala wa Trump, athari zake kwa walaji wa kawaida, sekta ya viwanda, na hata ukuaji wa
uchumi zinazidi kuwa wazi. Walaji wa kawaida ndio wanaoathirika zaidi kwani ushuru unafanya bidhaa kuwa ghali, na hivyo kuongeza mfumuko wa bei. Umoja wa Ulaya unasisitiza kuwa ushuru huu ni
hatari kwa ajira na ustawi wa kiuchumi, msimamo ambao unasisitizwa na Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen. HALI YA BIASHARA KATI YA MAREKANI NA UMOJA WA ULAYA Mwaka 2023, thamani ya
biashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani ilifikia euro trilioni 1.6. Lakini licha ya urari huu wa kibiashara, Trump anasisitiza kuwa umoja huo unanufaika zaidi. Data zinaonyesha tofauti
ya asilimia 3 tu kati ya mauzo ya nje ya Umoja wa Ulaya kwa Marekani na yale ya Marekani kwa Umoja wa Ulaya, jambo linaloibua maswali kuhusu msingi wa ushuru unaopendekezwa. Moja ya sekta
zinazolengwa zaidi ni sekta ya magari ya Ulaya. Cecilia Malmström anaonya kuwa magari kutoka Ujerumani, Sweden, na nchi zingine za Ulaya huenda yakawekewa ushuru mkubwa zaidi, hali inayoweza
kuongeza bei na kupunguza mauzo. Kampuni kama Volvo tayari zimeathirika kutokana na kupanda kwa gharama za chuma na alumini. HALI YA UHUSIANO KATI YA UJERUMANI NA MAREKANI To view this
video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video Soma pia:Je, China inaweza kuibuka kidedea katika vita vya kibiashara na Marekani? Hildegard
Müller, Rais wa Chama cha Sekta ya Magari ya Ujerumani, anatahadharisha kuwa ushuru wa asilimia 25 unaopendekezwa na Trump ni "uchokozi wa wazi” ambao utakuwa na athari mbaya kwa
uchumi wa Ulaya na Marekani. Katika kipindi chake kama Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya, Malmström alishiriki mazungumzo magumu na utawala wa Trump, na kufanikisha makubaliano ya
kupunguza ushuru mwaka 2020. Lakini safari hii, anasema hali ni ngumu zaidi kwa sababu ya kutotabirika kwa Trump. Malmström anasema kuwa mazungumzo yanapaswa kufanyika kwa haki kwa pande
zote mbili, lakini kwa sasa, kuna hofu kuwa Umoja wa Ulaya unaweza kulazimika kuchukua hatua za kulipiza kisasi. EU ITAVYOKABILIANA NA VITA VYA KIBIASHARA Kwa sasa, Umoja wa Ulaya unajiandaa
kwa uwezekano wa mgogoro wa muda mrefu. Chombo cha Umoja wa Ulaya cha kuzuia shinikizo la kiuchumi, ACI, ambacho kilianzishwa ili kukabiliana na China na kulinda maslahi ya umoja huo,
kinaweza kutumika kwa mara ya kwanza dhidi ya Marekani iwapo Umoja wa Ulaya utaona ushuru huu kama shinikizo la kiuchumi. Soma pia:Rais Trump kuzungumza na Waziri Mkuu wa Japan, Shigeru
Lakini je, kuna matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano? Malmström anasema hakuna anayependa vita vya biashara, na madhara yake yatakuwa makubwa kwa viwanda na wafanyakazi wa pande zote za
Atlantiki. Kwa sasa, dunia inasubiri kuona iwapo Umoja wa Ulaya na Marekani zitaepuka mgogoro mpya wa kibiashara, au kama ushuru huu utasababisha mtikisiko mwingine wa kiuchumi.