Play all audios:
Baraza la Maasofu chini Ghana wachangia 70,000 cedi za nchini humo katika Mfuko wa udhamini Kitaifa wa mapambano dhidi ya janga la Covid-19.Hatua hiyo kwa mujibu wa kiongozi mkuu wa Kanisa
nchini humo amefafanua kuwa Mpango ya Baraza la Maaskofu katika kujibu janga hilo utadumu kwa miezi tisa,kwa kusudi la kutoa vifaa vya kinga binafsi na kwa wafanyakazi wote wa vituo vya afya
Katoliki. NA SR. ANGELA RWEZAULA – VATICAN Siku ya Ijumaa Mei Mosi 2020, Baraza la Maaskofu nchini Ghana (GCBC) kwa kupitia Askofu Mkuu Charles Gabriel Palmer-Buckle, wa Jimbo Kuu Katoliki
la Cape Coast na Makamu Rais wa Baraza hilo GCBC,alikabidhi Hundi ya Cedi 70.000, fedha za Ghana ili kusaidia kuchangia Mfuko wa Kitaifa katika mapambano ya janga la COVID-19. MCHANGO HUO,
ULIKABIDHIWA KATIKA OFISI YA SEKRETARIETI KUU YA ACCRA, kwa ushiriki wa Padre Lazarus Anondee, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Ghana na msimamizi wa Mfuko wa udhamini ya
Kitaifa wa COVID-19, Dk. Collins Asare, pia Jude Kofi Bucknor, mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, kitaifa ambaye alishuhudia kupokelewa kwa hundi hiyo kwa niaba ya Mfuko huo kwa mujibu wa
taarifa iliyotolea katika ukurasa wa Facebook wa Jimbo kuu katoliki nchini Ghana. BWANA KOFI BUCKNOR, MJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI ameshukuru Kanisa kwa niaba ya wadhamini wote kwa mchango
wao wa ukarimu na amehakikishia kuwa pesa hiyo itatumika kwa uadilifu na uwajibikaji. 25/04/2020 Huduma ya Caritas nchini Ghana itaendelea kujibu mahitaji ya maskini na wengi wenye
mazingira magumu walioshambuliwa na janga la virusi vya corona,hata baada ya kumalizika ... KATIKA FURSA HIYO ASKOFU MKUU PALMER-BUCKLE AMEITUMIA PIA KUELEZA JUU YA MPANGO wa Baraza la
Maaskofu Ghana katika kujibu janga la Covid-19 na kwamba unachukua miezi tisa, na ambao unakusudia kutoa vifaa vya kinga vya binafsi na kwa wafanyakazi wote wa vituo vya afya Katoliki walio
mstari wa mstari wa mbele, pia vifaa vya misaada kwa wazee na watu walio katika mazingira magumu. Kwa kuhitimisha anatoa shukurani kubwa kwa wote hasa wafanyakazi walio mstari wa mbele kwa
kujitoa bila kujibakiza huku akiombea ulinzi na msaada kutoka kwa Mungu katika wakati huu mgumu.