Play all audios:
2024.02.12 Papa alikutana na wajumbe washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Chuo cha Kipapa cha Maisha, (Vatican Media) Baba Mtakatifu Papa Francisko:Teknolojia zijali kwanza kiini cha
mwanadamu Papa akikutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Chuo cha Kipapa cha Maisha,walioanza mkutano kuanzia Jumatatu 12-14 Februari 2024 kwa ajili ya kutafakari mtindo wa
kianthropolojia unaowianisha taaluma mbalimbali huku wakiepuka utawala wa kiteknolojia amesisitizia zaidi kuwa zana hizo mpya zisiharibu asili ya kina ya mwanadamu. Na Angella Rwezaula,
-Vatican
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 12 Februari 2024 alikutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Chuo cha Kipapa cha Maisha unaojikita na mada: "Binadamu: Maana na Changamoto"
ameanza kumsalimia mkuu wa Chuo hicho, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia na Askofu Mkuu mpya wa Santiago ya Chile, na kuwashukuru kwa kujitolea kwao kuendeleza utafiti katika nyanja za sayansi ya
maisha, afya na uponyaji, ahadi ambayo imeashiria kazi ya Kanisa, katika Chuo cha Kipapa cha Maisha kwa miaka hii thelathini ya kuwepo kwake. Swali wanalolizungumzia katika Mkutano Mkuu huu
ni la muhimu sana, yaani, jinsi tunavyopaswa kuelewa ni nini kinachomtofautisha binadamu. Ni swali ambalo ni la kale na bado jipya daima, ambalo rasilimali za ajabu zinazotolewa na
teknolojia mpya zinatuletea njia ngumu zaidi. Wenye maono daima wameweka wazi kwamba mtu hawezi kuchukua msimamo, mkuu ama 'kwa' au 'dhidi' wa mashine na teknolojia; kwa mujibu wa uzoefu
wetu wa kibinadamu, kinyume cha namna hiyo kinathibitisha kutokuwa na maana.
Papa alisalimiana na kila mmoja wa washiriki wa Mkutano wa Chuo cha Kipapa cha Maisha (Vatican Media) Baba Mtakatifu alisema kuwa leo hii pia, wito wa kutofautisha kati ya michakato ya
asili na ya bandia, kuona ule wa awali kuwa wa kibinadamu kihalisi na wa pili kuwa wa kigeni au hata kinyume na ule wa kibinadamu, huthibitisha vivyo hivyo kuwa hautoshi. Haifanyi kazi.
Kinachohitajika, badala yake, ni kuweka maarifa ya kisayansi na kiteknolojia ndani ya upeo mpana zaidi wa maana, na hivyo kuepusha hali ya juu ya dhana ya kiteknolojia (taz. Laudato Si',
108). Baba Mtakatifu ametoa mfano, jaribio la kumzalisha mwanadamu kwa njia na mbinu zinazotolewa na teknolojia. Mtazamo kama huo unajumuisha kupunguzwa kwa mwanadamu hadi kwa jumla ya
maonesho yanayoweza kurudiwa kulingana na lugha ya kidijitali ambayo inadhania kuwa kila aina ya habari inaweza kuoneshwa kwa kutumia lebo ya namba. Sambamba dhahiri na historia ya Biblia
ya Mnara wa Babeli (rej. Mwa 11:1-9) inaonesha jinsi hamu ya kuunda lugha moja imejikita sana katika historia ya wanadamu.
Kuingilia kati kwa Mungu, mara nyingi kufutwa kwa haraka kama adhabu tu, kunaweza kuonekana katika maneno chanya kama aina ya baraka, kama jaribio la kukabiliana na mwelekeo kupitia kuenea
kwa lugha za wanadamu. Kwa njia hii, wanadamu wangekabiliana ana kwa ana na mapungufu na udhaifu wao, na kupewa changamoto ya kuheshimu tofauti na kuonesha kujali wao kwa wao. Kwa hakika,
uwezo ulioongezeka wa sayansi na teknolojia unaweza kuwafanya wanadamu wajione wanajishughulisha na kazi ya uumbaji sawa na ile ya Mungu, na kuzalisha sura na mfano wa maisha ya binadamu,
ikiwa ni pamoja na uwezo wa lugha ambayo mashine za kuzungumza nazo, kuonekana amejaliwa. Kwa hiyo je kungekuwa ndani ya uwezo wa kibinadamu kuingiza roho ndani ya kitu kisicho hai?
Majaribu ni ya siri.
Papa akisalimiana na Askofu Mkuu Paglia (Vatican Media) Baba Mtakatifu Francisko akiendelea ambainisha kuwa Kinachoombwa kwetu ni kutambua jinsi ubunifu waliokabidhiwa wanadamu unavyoweza
kutekelezwa kwa uwajibikaji. Kwa maneno mengine, tunawezaje kuwekeza talanta tulizopokea huku tukizuia uharibifu wa kile ambacho ni binadamu na kufuta tofauti za msingi zinazotoa utaratibu
kwa ulimwengu (rej. Mwa 1-3). Kazi kuu, basi, ni ya anthropolojia: tunachangamoto ya kukuza utamaduni ambao, kwa kuunganisha rasilimali za sayansi na teknolojia, unaweza kutambua na kukuza
mwanadamu katika umaalumu wake usioweza kupunguzwa. Kuna haja ya kuchunguza kama umaalum huu unapatikana hata juu ya mkondo wa lugha, ndani ya nyanja ya pathos na hisia, tamaa na nia, ambayo
ni wanadamu pekee wanaoweza kuyaona, kuyathamini na kuyageuza kuwa mahusiano chanya na yenye manufaa na wengine, wakisaidiwa na neema ya Muumba. Hii hatimaye ni kazi ya kitamaduni, kwa kuwa
utamaduni huunda na kuelekeza nguvu za maisha na mambo mengine ya kijamii.
Pili, kwa jinsi mijadala yao ilivyopangwa, "tunaweza kuona mbinu ya kuendelea na sinodi, iliyorekebishwa ipasavyo kushughulikia mada hizo muhimu kwa dhamira ya Chuo. Utaratibu huu
unahitajika, kwa kuwa unahusisha uangalifu wa makini na uhuru wa roho, na utayari wa kuweka njia zisizojulikana na zinazojulikana, bila majaribio ya bure ya "kuangalia nyuma". Kwa wale
waliojitolea kwa upya wa mawazo na ys kiinjili, ni muhimu kutilia shaka hata maoni yaliyotulia na mawazo ambayo hayajachunguzwa kwa kina. Katika suala hili, Ukristo daima umetoa mchango
mkubwa, ukichukua vipengele vya maana kutoka kila utamaduni ambapo umekita mizizi na kutafsiri upya katika mwanga wa Kristo na Injili, kuchukua rasilimali za lugha na dhana zilizopo katika
mazingira mbalimbali ya kiutamaduni."
Zawadi kutoka kwa mmoja wa washiriki wa mkutano wa chuo cha Kipapa cha Maisha (Vatican Media) Baba Mtakatifu Francisko alisisitiza kuwa "Huu ni mchakato mrefu na unaoendelea unaohitaji
mbinu ya kiakili yenye uwezo wa kukumbatia vizazi vingi; inaweza kulinganishwa na hekima na maono ya wale wanaopanda miti wakijua kwamba matunda yao yataliwa na watoto wao, au wale
wanaojenga makanisa makuu wakijua kwamba yatakamilika na vizazi vijavyo. Ni mtazamo huohuo, ulio wazi na wa kuwajibika, na wa utulivu kwa Roho ambaye, kama upepo, huvuma upendapo (rej. Yh
3:8), ambayo ninamwomba Bwana awajalie ninyi nyote." Baba Mtakatifu Francisko aliwatakia kila baraka ili maoni na ushauri wao uwezi kutajirisha na kuzaa matunda. Aliwabariki kwa moyo
mkunjufu na kuwaomba, tafadhali, wakumbuke katika maombi yao.
Mchango wako kwa ajili ya utume mpana zaidi: tuunge mkono ili tupeleke ujumbe wa Papa kwa kila nyumba. 12 Februari 2024, 17:45 Tuma Chapa